Yanga na Simba Hakuna Mbabe, Vita ya Inonga na Mayele Yawa Kivutio

 

Kikosi cha Yanga kilichoanza dhidi ya Simba

PAMBANO la watani wa jadi kati ya Yanga ambaye alikuwa mwenyeji na Simba limemalizika kwa matokeo ya sare ya bila kufungana ikiwa ni pambano la raundi ya pili ya Ligi Kuu ya NBC msimu huu.

 

Katika mchezo huo uliotawaliwa na ufundi mwingi lakini pia uchache wa nafasi za mabao umelalamikiwa na wadau wengi wa soka kuwa ulikuwa ni mchezo ambao timu zote ziliangalia matokeo baada ya mchezo kuliko matokeo ndani ya mchezo, kwa maana zilicheza kwa tahadhari ya kuogopa matokeo ambayo yangeweza kupatikana mwisho wa mchezo

Mlinzi wa kushoto wa Simba Mohamed Hussein akiwa katika majukumu yake kwenye mechi ya dabi dhidi ya klabu ya Yanga

Kutokana na matokeo hayo klabu ya Yanga inaendelea kujikita kileleni ikiwa na jumla ya alama 55 ikifuatiwa na mahasimu wao klabu ya Simba ambayo ina jumla ya alama 42 ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

 

Baada ya mchezo huu klabu ya Yanga inatarajiwa kwenda mkoani Kigoma kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya klabu ya Ruvushooting unaotarajiwa uchezwa katika Uwanja wa Lake Tanganyika.

 Toa remark