Politics

Wachina Wapandishwa Kizimbani kwa Tuhuma za Uhujumu UchumiMamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewafikisha watuhumiwa wawili raia
wa China katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mkoani Dar es Salaam,
kwa makosa manne ikiwa ni pamoja na kukutwa na bidhaa ambazo hazijafuata
taratibu za forodha, kukwepa kodi na uhujumu uchumi.

Washtakiwa hao Zhu Wei na Tao Pan wamefikishwa katika mahakama hiyo
na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo Rita
Tarimo.

Wakili wa serikali kutoka TRA Emmanuel Medalakini amaedai
mahakamani hapo kuwa, watuhumiwa hao walikamatwa na mali hizo tarehe 13
mwezi huu katika eneo la Vingunguti mkoani Dar es Salaam ambapo
wanadaiwa kushindwa kutoa nyaraka za kuthibitisha uhalali wa mali
walizokutwa nazo.

Katika shtaka lingine, washtakiwa hao wanadaiwa kukwepa kulipa
kodi ya zaidi ya shilingi milioni 400 huku wakijua kufanya hivyo ni kosa
kisheria.

Baadhi ya bidhaa walizokamatwa nazo watuhumiwa hao ni vitenge, nyuzi
za kushonea,vitambaa vya mapazia na mabegi ya Kompyuta mpakato vyote
vikiwa vinatajwa kuingizwa nchini kwa njia ya magendo.

Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama ya Kisutu kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

Wakili Medalikini pia ameieleza mahakama kuwa, upelelezi wa shauri
hilo unaendela na uko mbioni kukamilika, hivyo washtakiwa hao
wamerudishwa rumande hadi tarehe 29 mwezi huu kesi yao itakapotajwa
tena.

Tangazo

ap

taboola dsk

ad

Advertisement

Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

Mgid

taboola apo chini

hapa

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published.