Mabalozi wa Sweden na Finland wamewasilisha rasmi maombi yao ya
kujiunga na Jumuiya ya Kujihami ya NATO leo kwa Katibu Mkuu Jens
Stoltenberg.
Hayo yamefanyika katika hafla ya video mjini Brussels.
Akiyakubali maombi hayo, Stoltenberg amesema hatua hiyo ni ya kihistoria
katika wakati muhimu sana kwa usalama wa Ulaya.
“Wanachama wa NATO sasa
watazingatia hatua zinazofuata kuelekea nchi zenu kuwa wanachama.
Usalama wa wanachama wote lazima uzingatiwe pia katika mchakato huu na
tunadhamiria kuangazia masuala yote na tupate suluhisho la haraka.”
Urusi imesema maombi hayo ya
Sweden na Finland kutaka kuwa wanachama wa NATO hayaleti tofauti yoyote
kwa kuwa nchi hizo zimekuwa zikishiriki luteka za kijeshi na muungano
huo wa kujihami.
chn
ap
taboola dsk
ad
Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )