guiness

Safari ya Mwisho ya Rais Banda

Rais Hakainde Hichilema wa Zambia, jana, Alhamisi, Machi 17, 2022 ameongoza waombolezaji kwenye mazishi ya Kitaifa ya Rais mstaafu wa Taifa hilo Rupiah Banda aliyefariki dunia tarehe 11 mwezi huu baada ya kuugua saratani ya tumbo kwa muda mrefu.


Katika mazishi hayo ya Kitaifa ya Banda, Tanzania imewakilishwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.


Mazishi rasmi ya Banda ambaye alikuwa Rais wa awamu ya nne wa Zambia yanatajiwa kufanyika hapo kesho, katika bustani ya Ubalozi kwenye makaburi ya Marais yaliyopo mji mkuu wa ‘Zambia, Lusaka.

Banda aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 85, ameiongoza Zambia kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2011.
Ni Rais wa tano wa Zambia kufariki dunia tangu Zambia ijipatie uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka 1964.


Toa remark