Rais wa Palestina Adai Kuipeleka Kesi ya Abu Akleh Mahakama ya ICC

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas

RAIS wa Palestina Mahmoud Abbas amedai anafikiria kuipeleka kesi ya mauaji ya mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji la Al- Jazeera Shireen Abu Akleh ili haki itendeke kwa mauaji ya kinyama yaliyotekelezwa na majeshi ya Israel.

 

Abu Akleh aliuawa na majeshi ya Israel wakati anaripoti habari juu ya ukatili na unyanyasaji wa raia wa Palestina waliopo kwenye kambi ya wakimbizi ya Jenin ambayo inashikiliwa na majeshi ya Israel.

Shireen Abu Akleh enzi za uhai wake

Abu Akleh alikuwa ni mwandishi wa habari mbobezi ambaye alifanikiwa kufanya kazi katika tasnia hiyo kwa takribani zaidi ya miaka 20, na alikuwa akiheshimika sana na jamii ya Wapalestina kutokana na mchango wake katika kuripoti habari za ukatili na unyanyasaji wa majeshi ya Israel ndani ya Palestina.

Wanajeshi wa Israel wakiwasambaratisha waombolezaji kwenye mazishi ya mwandishi wa habari Shireen Abu Akleh

Wakati wa mazishi yake wanajeshi wa Isarel walisababisha vurugu kwa kuwavamia na kuwasambaratisha waombolezaji waliokuwa wamebeba sanduku la kuhifadhia maiti ya Abu Akleh.

 Toa comment