Rais Samia Awasili Zanzibar Baada ya Kuhitimisha Ziara Yake Nchini Oman na Saudi Arabia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango, Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali waliofika kumpokea katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakati akitokea nchini Saudi Arabia mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya Kiserikali nchini Oman, tarehe 16 Juni, 2022.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili Visiwani Zanzibar mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi nchini Oman pamoja na Saudi Arabia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango, Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakati akitokea nchini Saudi Arabia tarehe 16 Juni, 2022 baada ya kuhitimisha ziara yake ya Kiserikali nchini Oman

Rais Samia akiwa nchini humo alifanikiwa kuhudhuria Kongamano la mkutano na wafanyabiashara wa Oman pamoja na wale Tanzania ambapo aliongelea juu ya kuimarishwa kwa mahusiano na mazingira mazuri ya biashara baina ya mataifa hayo, huku akibainisha kuwa yeye kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atahakikisha anatengeneza mazingira mazuri ya wafanyabiashara kuwekeza nchini na wale wa Tanzania kuangalia fursa za nini cha kufanya katika mataifa hayo.

 

 


Toa comment