Politics

Rais Samia aomba msaada kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi


By Juma Issihaka

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan, ameyaomba mashirika ya kimataifa kuzisaidia nchi zinazoendelea kuendana na kasi ya mabadiliko ya tabia nchi katika matumizi ya nishati ya kijani.

Samia ameyasema hayo leo Jumamosi Aprili 23, 2022 alipozungumza na Rais wa Benki ya Dunia, David Malpass kuhusu mitaji kwa wananchi.

Amesema ingawa ulimwengu unazitaka nchi kubadili matumizi ya nishati ili kuepuka uharibifu wa mazingira, lakini nyingi zinahitaji usaidizi ili kuendana na mabadiliko hayo.

 “Mashirika ya kimataifa yanakuja na teknolojia mpya kila siku, wanatwambia tutumie nishati ya kijani, mara tusifanye hivi mara tusifanye hivi.

“Lakini yanapaswa kuangalia hali tulizonazo, kwa sababu sasa tunatakiwa kwenda katika nishati ya kijani. Kwa mfano Afrika tunaweza kwenda katika gesi, umeme jua na upepo lakini tunahitaji msaada kukusanya nishati katika vyanzo hivyo,” amesema.

Katika mazungumzo yake hayo, Samia ameeleza juhudi zilizofanywa na Tanzania katika sekta ya elimu, ambazo ni kutoa huduma hiyo bila malipo kuanzia ngazi ya msdingio hadi sekondari na mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

Advertisement

Pia, amesema Tanzania imeondoa zuio la wanafunzi walioacha shule kwa sababu mbalimbali ukiwemo ujauzito na sasa wanaruhusiwa kuendelea na masomo.

“Kwa sasa wanapoacha wako huru kurudi shuleni na baadhi yao wanafanya vizuri tuna mfano Zanzibar. Zuio hili lilipoondolewa wapo waliofaulu na sasa wanahitimi vyuo vikuu,” amesema.

Ametaja changamoto katika sekta ya elimu ni uchache wa walimu na kwamba Serikali inaendelea kutoa ajira hiyo hasa wa sayansi kuhakikisha inatatua hilo.

Kuhusu usawa wa jinsia, Samia amesema awali Tanzania ilikuwa ikielimisha wanawake pekee kuhusu hilo, jambo lililosababisha kuendelea kutokea kwa matukio ya ukatili wa kijinsia.

“Lakini kwa sasa tumeshajua kumbe si wanawake pekee wanaopaswa kuelimishwa bali wanaume wanahitaji elimu hiyo ili jinsi zote ziwe na uelewa wa pamoja,” amesema Samia.Source hyperlink

Leave a Reply

Your email address will not be published.