Mwanasiasa Mkongwe wa Upinzani Nchini Uganda Kizza Besigye Akamatwa

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Dkt Kizza Besigye.

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Dkt Kizza Besigye alikamatwa Mei  25, 2022 alipokuwa akijaribu kuongoza maandamano katika mji mkuu, Kampala, kupinga gharama kubwa ya maisha.

Besigye mwenye umri wa miaka 66 aligombea urais dhidi ya Yoweri Museveni mara nne. Aliwahi kuwa daktari wa kibinafsi wa Rais Yoweri Museveni na amekamatwa mara nyingi.

Dkt Besigye alifika kwenye maandamano ya Jumanne akiwa na megaphone kwenye gari lake na kusimamisha shughuli za biashara katika eneo hilo, kulingana na tovuti ya habari ya Daily Monitor.

Polisi wa Uganda waliambia shirika la habari la Reuters kwamba wanamshikilia Dkt Besigye kwa tuhuma za kuchochea ghasia.

Besigye mwenyewe bado hajatoa kauli yake kuhusiana na suala hiloToa comment