Mtangazaji wa Wasafi FM Diva na Mumewake Apata Ajali ya Gari Usiku wa Kuamkia Leo

Mtagazaji wa Wasafi FM, Diva akiwa na na mumewake, Sheikh Abdulrazak salum.

MTANGAZAJI wa Wasafi FM, Diva amepata ajali ya gari usiku wa kuamkia leo Aprili 24,2022 akiwa na mumewake, Sheikh Abdulrazak salum baada ya gari walilokuwa wakiendesha kugongana na Bajaji.

 

“Diva ametoa taarifa hiyo kupita ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika “Asante kwa raia waliotusaidia with alot of affection maana i used to be devastated .. and thanks @iamnellyg5 Ni Mungu tu!. leo tunaendelea na matibabu …. maisha ya Mwanadamu ni mafupi sana nimeona jana. bajaj au Pikipiki wakiendelea achiwa wataendelea sababisha vifo vya wengi sana.

 

Siwez ata kulala naona ile bajaj ikipanda juu ya kioo cha gari and the blood … it was scary Mungu wangu🥲 ila Mungu anatupenda sana Kwa Ule mzinga tumetoka wazima Ni kudra zake mwenyezi Mungu na msaada tumepata kwa mapenzi sana makubwa ya watu .. nimepost kushukuru watu raia wa kawaida kabisa ambae walitu take care na kuhakikisha kila kitu chetu kiko salama na sisi tuko salama hatuna cha kuwalipa kabisa zaid ya shukran za upendo kwenu!.”amesema Diva.

Toa remark