Entertainment

Mayele apewa dozi usiku – MwanaspotiBy Khatimu Naheka

YANGA inashuka uwanjani leo katika mechi ya Ligi Kuu Bara, lakini kama kuna beki wa Namungo anajipanga kumzuia straika Fiston Mayele, anatakiwa kujiandaa sawasawa baada ya kocha mmoja kumuanzishia Mkongomani huyo dozi ya mazoezi maalumu ya usiku ili kumweka fiti zaidi ya alivyokuwa katika mechi 19 za awali za timu hiyo.

Namungo kutoka Lindi inayoshika nafasi ya tatu katika msimamo, imekuwa ngumu inapovaana na Yanga kwani katika mechi tano za Ligi Kuu imelazimisha sare, japo ilipasuka kwenye nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi mapema mwaka jana na makocha wa Jangwani ni kama wameshtuka na kumpika kinara wao wa mabao.

Yanga na Namungo, zitavaana leo saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa katika mechi ya ligi, ambayo pia itakuwa na vita baina ya Mayele na Reliants Lusajo wanaochuana kwenye mbio za ufungaji mabao, straika wa Yanga akiwa na mabao 11 na Lusajo ana 10, huku kila mmoja akiasisti matatu.

Ukiacha mazoezi ya kila siku na wenzake kuna mazoezi maalum magumu ameanza kupewa Mayele ambayo kama alikuwa hashikiki basi makali yake yataongezeka zaidi katika mechi zilizosalia.

Mayele amekuwa akifuliwa usiku na kocha wa mazoezi ya viungo Helmy Gueldich ambayo yamekuwa yakionekana makali huku ikishtua yakifanyika usiku.

Advertisement

Akizungumzia ratiba hiyo Helmy alisema mazoezi hayo yamekuwa maalum kwa baadhi ya wachezaji akiwemo Mayele ambaye amekuwa akiimarishwa ili aweze kuendelea kupambana na mabeki ili afunge zaidi.

Helmy ambaye ni beki wa zamani wa kushoto alisema mazoezi hayo amekuwa akipewa Mayele katika siku za kwanza za mwanzo wa wiki pekee na sio zaidi ili kumwondelea uchovu kutokana na bado anakuwa katika programu nyingine ya mazoezi na wenzake.

“Unajua inakuwqa kama Mayele ndio kielelezo kutokana na tunataka kumuimarisha zaidi, huyu ni mchezaji ambaye anakamiwa sana na kuna wakati mpaka wanamuumiza, sasa haya mazoezi ya usiku yanamuongezea uimara zaidi,” alisema Helmy na kuingeza.

“Watu watauliza kwanini usiku, unajua mchana Mayele amekuwa akifanya mazoezi na timu nzima sasa usiku kunakuwa na muda wa kujifua zaidi pale kwenye chumba cha gym.”

Aidha, Helmy aliongeza mbali na Mayele ratiba hiyo pia imekuwa ikiwahusisha kiungo Feisal Salum, mawinga Farid Mussa, Chico Ushindi na mshambuliaji Yacouba Songne ambaye amekuwa na ratiba kama hizo za mara mbili kwa siku.

“Kuna Ushindi (Chico) pia naye amekuwa katika ratiba kama hii, nilikwambia mapema kwamba huyu Ushindi ni suala la muda tu atashangaza wengi.”

Source hyperlink

Leave a Reply

Your email address will not be published.