Mapacha Wenye Miaka 9 Mkoani Arusha Wanaishi kwa Kula Magodoro

Mama mzazi wa watoto hao, Joyce Mrema amesema tatizo lao lilianza wakiwa na umri wa miaka mitatu

Mapacha wenye umri wa miaka 9 mkoani Arusha wanaoishi huku wanakula magodoro, wanaomba msaada ili wakatibiwe.

 

Mama mzazi wa watoto hao, Joyce Mrema amesema tatizo lao lilianza wakiwa na umri wa miaka mitatu, ambapo walipowafikisha hospitalini madaktari walieleza kuwa hali hiyo inatokana na upungufu wa madini mwilini.

 

Mzazi huyo anasema kutokana na kipato chake kuwa cha chini, Joyce ameshindwa kuwahudumia watoto hao ipasavyo , ambapo yupo eneo la Sokoni One, Arusha.

 

Anasema awali alikuwa akiishi na baba wa watoto hao, lakini alitoweka kutokana na deni la Sh milioni tatu, hivyo kupelekwa mahakamani, ingawa hakufafanua kuhusu jambo hilo.

 

Amesema kutokana na hali hiyo anaomba msaada ili aweze kuwapeleka hsopitali watoto hao, waweza kupata tiba. “Kwa watakaoguswa wanaweza kuwasiliana kwa namba yangu Joyce Mrema 0763876313, “ amesema.Toa comment