Entertainment

Manula akatwa na kioo – MwanaspotiBy Ramadhan Elias

WAKATI Simba ikiwa uwanjani CCM Kirumba, Mwanza ikiendelea na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Geita Gold, imetoa taarifa ya kipa wake Aishi Manula kukatwa na kioo.

Taarifa hiyo iliyochapishwa kwenye mitandao rasmi  ya klabu hiyo imeeleza kuwa Manula aliumia wakati akijiandaa na mechi hiyo.

“Dakika chache kabla ya kuanza kwa mchezo wetu dhidi ya Geita Gold, mlinda mlango wetu Aishi Manula aliumia mkono baada ya kukatwa na kioo katika chumba cha kubadilishia nguo ‘Dressing room’’. ilisema taarifa hiyo na kuongeza;

“Manula aliwasili uwanjani CCM kirumba akiwa kwenye orodha ya wachezaji wanaocheza mchezo wa leo na baada ya kuingia katika chumba cha kubadilishia nguo akaangukiwa na kioo ambacho kilivunjika baada ya kuegemewa na mashabiki waliokuwa nje ya chumba hicho”.

“Tayari Manula amepatiwa matibabu na anaendelea vizuri. Tutaendelea kuwajuza hatua kwa hatua ya maendeleo yake.” Ilieleza taarifa hiyo.

Baada ya Manula kuumia, kipa namba mbili wa wekundu wa msimbazi hao, Beno Kakolanya ndiye alichukua nafasi yake.

Advertisement

Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published.