Politics

Makamu Wa Rais Apokea Gawio La Serikali Kutoka Nmb June 15Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ameagiza Mashirika
ambayo Serikali ina hisa kuhakikisha yanaanza kutoa Gawio kwa serikali
mara moja, pia Taasisi zinazotakiwa kutoa asilimia 15 ya mapato ghafi
kwa mujibu wa sheria zifanye hivyo kikamilifu na kwa wakati.

Makamu wa Rais amesema hayo
wakati wa hafla ya kupokea Gawio la shilingi bilioni 30.7 kutoka kwa
Benki ya NMB iliofanyika katika Ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma tarehe 15 Juni 2022. Amesema Mashirika ambayo yanategemea ruzuku kutoka
mfuko mkuu wa Serikali yanapaswa kuwa na  mikakati madhubuti na
inayotekelezeka ya kupunguza utegemezi kwa Serikali na kumuagiza 
msajili wa Hazina kuhakikisha  wakuu wa taasisi husika wanatekeleza
maagizo hayo.


Aidha Makamu wa Rais amesema
Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuimarisha na kuweka mazingira
rafiki na endelevu ya kufanya biashara katika sekta ya fedha na sekta
zote nchini. Pia ameipongeza Benki ya NMB kwa kuendelea kuchangia
maendeleo ya jamii nchini (corporate social responsibility) sambamba na
kusaidia ukusanyaji wa mapato ya Serikali na kuimarisha mifumo ya
ukusanyaji mapato. Amewaasa kuendelea kushirikiana na Serikali katika
kuongeza fursa za ajira kwa vijana na wanawake pamoja na kuboresha
 huduma za kijamii kwenye sekta mbalimbali kama afya,elimu na utunzaji
wa mazingira ikiwa ni pamoja na  kukabiliana na athari za mabadiliko ya
tabianchi na tabiawatu.


Kwa Upande wake Waziri wa
Fedha na Mipango Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Wizara
itaendelea kusimamia maelekezo ya kuhakikisha taasisi za serikali na
zile ambazo serikali ina hisa zinatoa Gawio. Aidha amesema serikali
itaendelea kushirikiana na taasisi zote za sekta binafsi ili kuweza
kuhakikisha zinafanya kazi vizuri.


Awali Afisa Mtendaji Mkuu wa
Benki ya NMB Ruth Zaipuna amesema Gawio la Serikali kutoka Benki ya NMB
limeendelea kukua kila mwaka na kuwa endelevu mpaka kufikia bilioni 30.7
kwa mwaka 2022 kutoka bilioni 10.48 mwaka 2018. Amesema adhma ya NMB ni
kuleta tija kwa wawekezaji ikiwemo serikali ambayo inamiliki hisa za
asilimia 31.8.


Aidha Bi Zaipuna ameongeza
kwamba Benki ya NMB itaendelea kuwa mdau mkubwa wa serikali katika
kufanikisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi hasa kupitia uwekezaji
katika sekta ya kilimo na biashara. Amesema mpaka mwezi Desemba 2021
jumla ya mikopo ya shilingi Trilioni 4.3 imetolewa kwa wakulima na
wafanyabiashara.

Tangazo

ap

taboola dsk

ad

Advertisement

Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

Mgid

taboola apo chini

hapa

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published.