Politics

Kikongwe aliyenusurika ajali ya moto Simanjiro afariki dunia


By Joseph Lyimo

Simanjiro. Kikongwe Anna Kipututu (70) ambaye alijeruhiwa kwenye ajali ya moto iliyoua watoto wanne wa Kijiji cha Ngage, Kata ya Loiborsoit Wilayani Simanjiro mkoani Manyara naye amefariki dunia na kuzikwa kijijini kwao.

Kipututu na wajukuu zake wanne waliungua ndani ya nyumba kwenye ajali ya moto baada ya kumwagia petroli kitandani na kuchoma moto ili kuwaua kunguni.
Diwani wa kata ya Loiborsoit, Siria Kiduya akizungumza na Mwananchi digital leo Mei 18, amesema Kipututu ambaye alikuwa anapatiwa matibabu Hospitali ya KCMC mkoani Kilimanjaro amezikwa Mei 17.
Kiduya amesema baada ya ajali hiyo kutokea Mei 3 na kusababisha vifo vya watoto wanne na bibi yao Kipututu kujeruhiwa kwa moto huo alilazwa hospitali ya KCMC ya mjini Moshi kwa ajili ya matibabu.

Ametaja watoto waliofariki dunia kwenye ajali hiyo ni  Jackson Mathayo (11) Sioni Raphael (9) Napokei Raphael (7) na Sifa Mathayo (5).

“Tunawashuku wananchi wote waliojitokeza kwa wingi kwenye mazishi na kujitoa kwani mmewapa faraja wafiwa,” amesema Kiduya.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Benjamin Kuzaga ametoa wito na ushauri kwa jamii wanapata ushauri kwa wataalamu wa mifugo ili kutumia dawa za kuulia wadudu.Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published.