Entertainment

Kapombe aumia – MwanaspotiBy Damian Masyenene

Mlinzi wa kulia wa Simba, Shomari Kapombe ameshindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia katika dakika ya 19.

Kapombe aliumia katika harakati za kuokoa mpira wakati Geita Gold ikifanya shambulizi langoni mwa Simba ambalo lilizaa bao likifungwa na George Mpole.

Baada ya kuanguka Kapombe alishindwa kuendelea na mchezo huo na kulazimu benchi la ufundi la Simba kufanya mabadiliko katika dakika ya 23.

Katika mabadiliko hayo, kinda Jimmyson Mwanuke ameingia kuziba nafasi ya Kapombe.

Mwanuke anacheza kama mlinzi wa  kulia nafasi ambayo aliitumikia vyema katika mchezo wa robo fainali ya kombe la Shirikisho dhidi ya Pamba akicheza dakika zote 90.

Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published.