Entertainment

Ishu ya Saido kuchelewa uwanjani iko hiviBy Thomas Ng’itu

MSHAMBULIAJI Saido Ntibazonkiza wa Yanga hakuwepo kabisa katika mstari wa wachezaji wenzake wakati wanasalimiana kabla ya mchezo dhidi ya Simba kuanza.

Wakati wachezaji wote wanaingia uwanjani na kwenda kujipanga ili mpira uanze, Ntibazonkiza yeye alichelewa kabisa kuingia uwanjani na walipokuwa wanasalimiana yeye alitoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na kwenda kwenye benchi la Yanga.

Wenzake waliposalimiana na kwenda kujipanga kwa ajili ya picha ya pamoja mchezaji huyo bado alikuwa pembeni kwenye benchi.

Mpira ulipowekwa kati Ntibazonkiza aliingia ndani haraka na kwenda kucheza sambamba na wenzake akitokea upande wa kushoto.

Ntibazonkiza alipoingia uwanjani hakuonyesha kuwa na majeraha ambayo yalimfanya akose kusalimiana na wenzake pamoja na picha ya ukumbusho.

Source hyperlink

Leave a Reply

Your email address will not be published.