Entertainment

Geita Gold yaja na staili mpya uwanjaniBy Damian Masyenene

WACHEZAJI wa Geita Gold wameingia kwa namna ya aina yake katika eneo la kuchezea la uwanja wa CCM Kirumba.

Wachezaji hao wametoka vyumbani kwa ajili ya kupasha misuli (warm up) wakienda moja kwa moja kwenye kona ya eneo ambalo Simba wamepanga vifaa vyao kwa ajili ya Warm up kisha kuanza kusambaa Uwanjani wakipita katikati ya ngome ya Simba.

Licha ya kuingia mapema Uwanjani saa 7:56 mchana Geita Gold walitulia vyumbani huku Simba walioingia saa 8:28 mchana wakiwa wa kwanza kupanga program zao za mazoezi.

Hata hivyo baada ya Makocha wa Simba kupanga program zao walirudi vyumbani kisha wachezaji wa Geita Gold kutoka na kuingia eneo la kuchezea (pitch) kwa mtindo huo.

Wachezaji wa Simba nao wameingia kuanza Warm up saa 9:14 wakianza kwa kutengeneza umbo la duara kisha kuanza mazoezi.

Mchezo huo utaanza saa 10 jioni katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa

Advertisement

Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published.